Kwa wanafunzi wote na wazazi
Habari.
Tunatumai mnaendelea vizuri na muu wazima wa afya.
Ukiachilia mbali matokeo yanayotumwa kwa wazazi kwa njia ya posta kuja kwa wazazi,tumeongeza njia nyingine ya kuhakikisha wazazi wanafahamu kuhusu matokeo ya watoto wao.
Njia ya kwanza nikupitia telegram channel ya shule,kama mzazi anasimu za kisasa anaweza download Telegram na kujiunga na channel ya shule ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu shule kama ratiba,mipango,matokeo n.k
Kama una telegram app tayari unaweza kujoin kwa kupitia link ifuatayo.
Link 1:Telegram https://t.me/MaraSecondaryschool
Njia ya pili ni kupitia blogspot ya shule,unaweza kuitafuta kwa jina lifuatalo marasecondaryschool.blogspot.com au kwa kufwatilia link ifuatayo
Link 2:Blogspot https://marasecondaryschool.blogspot.com
Njia ya tatu ni kupitia facebook page yetu ambayo kwasasa haipo tayari itakapokuwa tayari tutawafahamisheni.
Kama shule tunawaomba wazazi muwasaidie wanafunzi kwa kuwanunulia vitabu kwa masomo wanayoyasoma na pia kufwatilia mwenendo wa tabia na matokeo yao.Tafadhali kama mzazi usipopata matokeo ya mwanao wasiliana na shule kwa msaada zaidi.
Tunaimani kwa njia hii tutapunguza pengo kubwa la mawasiliano kati ya wazazi na shule ukizingatia hakuna vikao kati ya wazazi na shule vinavyofanyika mara kwa mara kutokana na umbali wa wazazi walipo.
Tunatoa shukrani kwa wazazi wote ambao wamekuwa wakifwatia mienendo ya watoto wao pindi wawapo shuleni tunaomba wazidi kufanya hivyo kwa kuhakikisha watoto wanapotoka nyumbani kuja shuleni wanafika shuleni kwa wakati.
Tunawatakia wanafunzi wote likizo njema na pia wasisahau kuendelea kusoma kwa bidii huku wakijiepusha na maambukidhi ya ukimwi pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya.
Asante.
Administration
Mara Secondary School
P.O Box 193,
Musoma,Tanzania.
Email:Marasecondary129@gmail.com
Comments
Post a Comment